Wednesday, July 13, 2016

Swansea wanataka kupanda dau kumsajili

 Leonardo Ulloa, kutoka Leicester.
Kanu

Swansea wanataka kupanda dau kumsajili Leonardo Ulloa, 29, kutoka Leicester, wakati wakijiandaa kwa kuondoka kwa Andre Ayew na Bafetimbi Gomis (Daily Telegraph), mshambuliaji wa Wales Hal Robson-Kanu ambaye ni mchezaji huru amepewa mshahara wa pauni 100,000 kujiunga na Ligi Kuu ya China (Daily Mirror).
Negredo kurejea tena england?
Negredo

Liverpool na Tottenham hawajakatishwa tamaa na bei ya pauni milioni 25 iliyowekwa kwa beki wa Kols, Jonas Hectors, 26 (Bild), Middlesbrough waliopanda daraja wanataka kumsajili beki wa Chelsea Tomas Kalas, 23 (Daily Express), Middlebrough pia wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Valencia Alvaro Negredo, 30, aliyeichezea Manchester City kwa misimu miwili (Guardian).

Chelsea kulipa  zaidi ya pauni milioni 50

  usajili wa beki Kalidou Koulibaly

toka  Napoli.
Morata

Chelsea wana wasiwasi kuwa huenda wakalazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 50 kumsajili beki Kalidou Koulibaly, 25, kutoka Napoli (Evening Standard), Real Madrid wameingia kwenye mbio za kumsajili kiungo wa Valencia Andre Gomes anayefuatiliwa na Chelsea (Fichajes), Madrid wameamua kutomuuza mshambuliaji wao, Alvaro Morata, 23, kwenda Chelsea (Daily Mail).
Manchester United tayari kumsajili kiungo 

kutoka Spain, Cesc Fabregas.

Fabregas
Fabregas kuungana tena na Mourinho?
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kumsajili kiungo kutoka Spain, Cesc Fabregas, 29, ambaye alikuwa naye Chelsea (Daily Mirror), Mourinho huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Newcastle, Moussa Sissoko, 26, iwapo atashindwa kumsajili Paul Pogba kutoka Juventus (Le 10 Sport), Man United wanaendelea kumfuatilia beki wa West Ham, Reece Oxford, 17 (Evening Standard), meneja msaidizi wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs, 41, atacheza katika ligi kuu ya India mwezi huu (Daily Mail).

John Stones wa Everton atangaza

 kujiunga na  Manchester City

Stones
John Stones
Mshambuliaji Wilfried Bony, 27, anajiandaa kuondoka Manchester City, huku Galatasaray wakitoa pauni milioni 3 za kumsajili kwa mkopo (Sun), Leroy Sane, 20 anayesakwa na Manchester City, hajaiambia klabu yake ya Schalke kuwa anataka kuondoka, wakati meneja mpya wa City Pep Guardiola akiwa tayari kutoa pauni milioni 40 kumsajili kiungo huyo Mjerumani (Daily Star).

Sunday, July 10, 2016

URENO MABINGWA ULAYA 2016

Ronaldo
Ureno wameshinda michuano ya kandanda ya Ulaya, Euro 2016, kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali mjini Paris.
Goli la ushindi lilifungwa na Eder katika dakika ya 110, na kusababisha huzuni kubwa kwa mashabiki wa Ufaransa waliofurika kwenye uwanja wa Stade de France.
Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Ureno. Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa.
Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana na kupata jeraha la goti katika kipindi cha kwanza.
Ufaransa ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuweza kuzitumia vyema nafasi walizopata.