Tuesday, May 10, 2016

Sanders amshinda Clinton mchujo wa West Virginia

Vyombo vya habari nchini Marekani vimebashiri kuwa mgombea wa tiketi ya chama cha Democratic kwa ajili ya uchaguzi wa urais Bernie Sanders ameshinda kura ya mchujo katika jimbo la West Virginia.
Hata hivyo mpinzani wake Hillary Clinton bado anashikilia uongozi kwa jumla katika kinyang'anyiro cha kugombea tiketi ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment